Real Madrid wamekamilisha usajili wa Kipa Arrizabalaga kwa mkopo wa msimu mzima kutoka Chelsea.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alikosekana uwanjani wakati Chelsea ilipotoka sare ya siku ya ufunguzi dhidi ya Liverpool Jumapili kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.
Kepa atatumika kama mbadala wa kipa chaguo la kwanza wa Madrid, Thibaut Courtois, ambaye alipata jeraha la ACL siku chache kabla ya msimu mpya na inasemekana atakuwa nje kwa muda mwingi wa msimu wa 2023-24.
Kipa alijiunga na Chelsea mwaka 2018 kwa euro milioni 80, mkataba ambao ni rekodi ya dunia kwa mlinda mlango.
Alicheza mechi 163 kwa The Blues, na kushinda mataji manne, pamoja na Ligi ya Mabingwa mnamo 2021.