Tetemeko la ardhi latikisa California wakati dhoruba 'Hilary' ikisababisha mafuriko makubwa

Magari ya kuzima moto yanaonekana katika eneo lililokumbwa na tetemeko la ardhi Kaskazini mwa mji wa Los Angeles.

Wakati eneo la Kusini mwa jimbo la California likikumbwa na dhoruba isiyo ya kawaida ya msimu wa  kiangazi Jumapili alasiri, tetemeko la ardhi la kipimo cha 5.1, cha rikta, pia liligonga eneo hilo, kwa mujibu wa idara ya Jiolojia ya Marekani.


Shirika la habari la CNN liliripoti Jumapili jioni kwamba Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa ni eneo la Ojai, kati ya miji ya Santa Barbara na Ventura, likiinukuu idara hiyo.


Hakukuwa na ripoti za mara moja za uharibifu, Sheriff wa Kaunti ya Ventura alisema katika ujumbe uliochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.


Awali, mafuriko makubwa yalikumba mitaa kadhaa katika eneo kame la Mexico la Baja California, siku ya Jumapili wakati Dhoruba Hilary iliposonga ufukweni ikisababisha mvua kubwa, ikielekea Kusini mwa California, na kusababisha wasiwasi kuongezeka kwamba mafuriko makubwa huenda yakatokea katika maeneo ya kaskazini kama jimbo la Idaho.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii