Mashambulizi ya makombora yasababisha vifo vya watu 20 Sudan

Takribani raia 20 wa Sudan wameuawa katika mashambulizi ya makombora yaliyorushwa katika maeneo ya makaazi ya mojawapo ya miji muhimu ya Darfur na karibu na hospitali katika jimbo la Kordofan Kaskazini.

Chama cha Madaktari kilisema kwamba tangu mapema siku ya Ijumaa, makombora yalirushwa karibu na hopsitali nne katika mji mkuu wa jimbo la Kordofan Kaskazini na kuwaua raia wanne na wengine 45 walijeruhiwa.

Katika mji mkuu wa jimbo la Darfur wa Nyala, chama cha wanasheria kimethibitisha vifo vya watu 16 vilivyosababishwa na shambulio la kombora.

Mkoa wa Darfur ambao tayari umegubikwa na mzozo mbaya katika miaka ya 2000, umeshuhudia ghasia mbaya tangu mapigano yalipozuka katikati ya mwezi wa nne baina ya Majenerali hasimu wa Sudan wanaowania madaraka.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii