Ndege ya kijeshi iliyokuwa na marubani wawili imeanguka ndani ya Ziwa Victoria, hatua chache kutoka Uwanja wa Ndege wa Bukoba.
Tukio hilo limetokea saa 3:30 asubuhi leo Julai 20, 2023 kuibua hofu na taharuki miongoni mwa wakazi wa Manispaa ya Bukoba ambao wamerejewa na kumbukumbu ya tukio la ndege ya abiria ya kampuni ya Precision Air kuanguka ndani ya Ziwa Victoria na kusababisha vifo vya watu 19 na majeruhi 26.
Katika tukio hilo la Novemba 6, 2022 ndege hiyo ya Precision Air namba ATR 42-5H PWF ilianguka baada ya marubani kushindwa kuona njia ya kutua kutokana na hali mbaya ya hewani.