Azam FC kuzindua leo jezi za msimu wa 2023/24

Matajiri wenye Jiji lao wasiokuwa na mbamba @azamfc leo wanatarajia kuzindua jezi zao mpya kwaajili ya msimu wa 2023/24.

Wauza lambalamba na Waoka Mikate hao wa @azamfc wameahidi uzi huo mpya kuanza kupatikana kwenye maduka saa 10:00 alasiri

”Baada tu ya uzinduzi, mtoko huo wa bara la Afrika utaingia sokoni na kuanza kuuzwa kuanzia saa kumi jioni. Mzigo utapatikana kwenye maduka yetu yaliyopo Kariakoo; makutano ya mitaa ya Livingstone na Aggrey, pamoja na klabuni Azam Complex Chamazi. Afrika itapendeza kuanzia Tanzania hadi Sousse Tunisia!.”- Taarifa kutoka Azam FC.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii