Amtema Mchumba Kisa Kujiunga na Shule ya Uuguzi

Mwanaume kutoka Ghana amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kufunguka sababu ya kuvunja uhusiano na mpenzi wake. 

mwanaume huyo, ambaye alionekana kuwa na hasira, alimweleza rafiki yake kuwa mpenzi wake, ambaye alikuwa amehitimu shule ya upili, hivi karibuni alimjulisha uamuzi wake wa kuendelea na masomo. 

“Najua mamake hana uwezo wa kifedha, kwa hivyo atategemea mimi kulipa karo yake. Anafikiri mimi ni mjinga. Nilimwambia sina pesa za kugharamia masomo yake, kwa hivyo anapaswa kusahau, hilo” alisema. 



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii