Tukio limetokea usiku wa kuamkia Julai 19, 2023 Mkoani #Arusha, ikielezwa Mtuhumiwa alienda Kanisani kumgongea mlango Padri Pamphilius Nada wa Parokia ya Karatu ili amuombee
Baada ya Padri kufungua mlango Mtu huyo akamvamia na kumpiga kwa Nyundo kichwani, kitendo ambacho kilikatisha uhai wake muda mfupi baadaye
Kamanda wa Polisi, Justine Masejo, amesema “Mtuhumiwa inadaiwa alikuwa na changamoto ya Afya ya Akili, naye alifariki baada ya kushambuliwa na Wananchi eneo la tukio.”