Mlinzi wa Raila Odinga Atekwa Nyara na Watu Wasiojulikana, Viongozi wa Azimio Wadai

Mlinzi wa Raila, Maurice Ogeta, alidaiwa kutekwa nyara na watu wasiojulikana akiwa amevalia mavazi ya kawaida. Katika taarifa, Philip Etale, mkurugenzi wa mawasiliano wa Chama cha ODM, alidai Ogeta aliwekwa kwenye buti ya gari na watu wanaoaminika kuwa wapelelezi kutoka Kurugenzi ya Upelelezi wa Jinai (DCI). 


"Watu wasiojulikana waliovalia mavazi ya kawaida wanaoshukiwa kuwa maafisa wa polisi kutoka DCI wamemteka nyara mlinzi wa Raila Odinga Maurice Ogeta alipokuwa akiendesha gari kuelekea kazini, wakamfunga kwenye buti ya gari na kumpeleka kusikojulikana. Mahali alipo bado hajulikani aliko," Etale alisema. 


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii