Vikosi vya usalama Kenya vyaua al-Shabaab 60

Vikosi vya usalama vya Kenya vimewauwa karibu wapiganaji 60 wa kundi la itikadi kali za kiislamu la al-Shabaab

Waziri wa Mambo ya ndani wa Kenya Kithure Kindiki amesema kuwa askari wa Kenya walikabiliana na wanamgambo hao kaskazini mashariki mwa Kenya katika eneo la Tana River.


Kindi amesema wapiganaji hao waliyalenga mabasi ya abiria, lakini vikosi vya usalama vilivyokuwa vimeshika doria vilijibu haraka shambulizi hilo na kuwauwa wanamgambo wote.

Raia wawili waliuawa katika shambulizi hilo. Kumekuwa na mashambulizi ya mara kwa mara kaskazini mwa Kenya ya kundi la al-Shabaab ambalo linaendesha harakati zake katika nchi jirani Somalia.

Mapema Julai, vikosi vya usalama vya Kenya viliwauwa wapiganaji 20 wa kundi hilo katika shambulizi sawa na hilo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii