Mshambuliaji mpya wa Young Africans, Hafiz Konkoni, ametamba kuisaidia Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans kufanya vizuri, ili kutetea mataji na kutikisa vilivyo kwenye Michuano ya Kimataifa msimu ujao 2023/24.
Konkoni aliyetia saini mkataba wa miaka miwili kuichezea Young Africans, amejiunga na klabu hiyo na kuziba pengo la FĂstone Mayele, aliyetimkia Pyramid ya Misri baada ya msimu uliopita kumaliza akiwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Msimu uliopita, mrithi huyo wa Mayele alifunga mabao 15 katika ligi ya Ghana baada ya kucheza mechi 26 na kutoa pasi tatu za mabao huku akishika nafasi ya pili kwa ufungaji.