Mwanamume mwenye umri wa miaka 56 atatumikia kifungo cha jela kwa miaka 15 ijayo baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mkewe.
Crispin Nyaga mwenye umri wa miaka 56 alimuua mkewe, Catherine Mbuya, siku ya Krismasi ya mwaka jana baada ya mzozo kati yao. Jalango made me cry after his official endorsement live on air Keep Watching Kilichosababisha ugomvi ilikuwa chakula; Nyaga alimshutumu mkewe kwa kukosa kununua nyama aliyokuwa amemtaka kutayarisha kwa ajili ya familia. Runinga ya Citizen iliripoti kwamba mwanamume huyo aliondoka nyumbani Desemba 25, 2022, kwenda kufanya sherehe.