Wazazi wametaka uchunguzi ufanywe baada ya mwanafunzi wa shule ya upili ya Kajiunduthi eneo bunge la Maara kupatikana amefariki katika eneo la River Maara jirani.
Wanafunzi hao wanadaiwa kuanza kuzozana na naibu mkuu wa shule mnamo Jumatatu, Julai 24 na kusababisha mgomo tena.
Wanafunzi walifanya fujo mwendo wa saa nane usiku na kuwalazimu uongozi wa shule kupiga simu katika Kituo cha Polisi cha Kaunti Ndogo ya Muthambi ili kupata usaidizi wa kudhibiti mgomo huo.