Petroli yaadimika Kiteto, lita yauzwa sh 6000

Mafuta ya petroli wilayani Kiteto mkoani manyara ambayo awali yalikuwa yakiuzwa kwa shilingi 2,930 kwa lita sasa yanauzwa shilingi 6,000 kwa lita baada ya kuadimika.

Hali hii imeanza kuathiri wananchi ambao wengi wao wanatumia usafiri wa bodaboda na hata magari binafsi kutokana na kuuzwa gharama.

Mji wa Kibaya ambao una vituo vitatu vya nishati hiyo ya mafuta kwa sasa vituo hivyo havina tena mafuta hayo na haijulikana yataletwa lini ikiwa leo ni siku ya pili kwa wananchi hao kuuziwa petrol hiyo kwa gharama kubwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii