Maandamano yaliyoitishwa na kiongozi wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga yaligeuka kuwa ya vurugu huku polisi wakikabiliana na waandamanaji katika maeneo mbalimbali nchini.
Maandamano ya Jumatano, Julai 12, yaliacha uharibifu mkubwa wa mali katika miji mikubwa kote nchini. 2023 Emmy Nominations Keep Watching Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome alikuwa ametangaza maandamano hayo kuwa haramu, jambo ambalo liliweka msingi wa makabiliano na wafuasi wa upinzani. Wakati wa mzozo huo, waandamanaji wanaoipinga serikali waliwasha moto barabarani huku polisi wakitumia kila njia kuwatawanya.
Kulingana na runinga ya Citizen, mapigano hayo makali yalisababisha vifo vya watu tisa kote nchini, huku zaidi ya 33 wakijeruhiwa huku wengine kadhaa wakikamatwa. Katika mji wa Mlolongo, watu wanne walidaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakijaribu kuwazuia waandamanaji kuharibu barabara ya Nairobi Expressway. Katika eneo la Kitengela, watu wawili waliuawa kufuatia makabiliano kati ya maafisa wa polisi wa kupambana na ghasia na waandamanaji.