Kwenye harusi za jadi za Igbo, ni desturi bwana harusi kupokea mvinyo kutoka kwa bibi harusi.
Anaunywa na kucheza kwa madaha na mkewe mtarajia ili kupokea baraka za ndoa baada ya kuweka pesa kwenye chombo kinachotumika kuleta kinywaji hicho.
Hata hivyo mambo yalikuwa tofauti katika harusi ya jadi ya hivi karibuni, na hii ilisababisha mjadala mkali mtandaoni.
Wakati ulionaswa kwenye kamera na mwanamke fulani, ulionyesha bwana harusi akimwaga mvinyo huo chini baada ya bibi harusi kumpa.
Kisha alisimama na kusonga mbele na mrembo huyo, ambaye alionekana kutokujali kitendo chake cha kutokunywa mvinyo huo. Mwanamke huyo, aliyeshiriki video hiyo, alijiuliza kwa nini bwana harusi alikataa kunywa mvinyo wa kokonati kama ilivyodaiwa na desturi ya harusi.