Maafisa wa upelelezi wameanzisha uchunguzi kuhusu kisa ambapo mwanamume mmoja alifariki kwa kujitoa uhai baada ya mkewe kuripotiwa kukataa kumpikia kuku nyumbani kwao Uriri, kaunti ya Migori.
Huku akithibitisha kisa hicho cha kushangaza, Chifu wa Nyaobe John Atonya alisema mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 45 alijifungia ndani ya nyumba yao kabla ya kujiteketeza. “Mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina la John Rugala alijifungia ndani ya nyumba kabla ya kuiteketeza. Inadaiwa kuwa mke alikataa kumpikia kuku,” Atonya alisema.