Jamaa Ahuzunika Baada ya Mkewe Kutoroka na Mwanaume Mwingine Siku ya Harusi Yao

kijana mmoja kuoa na kuwa na familia yake zilivunjwa na mwanamke ambaye alikuwa amemwamini.

Mwanamume huyo mwenye huzuni alisalia amechanganyikiwa na mumeza mate machungu baada ya ndoa yake kuvunjika siku ya harusi yake na barafu wake wa moyo.

Uwihoreye Francois alisema kuwa mkewe alimchiti siku yao maalum, akimwacha na uchungu na huzuni kubwa. "Nilimwacha mke nyumbani Butare. Mara tu baada ya kuondoka, alitoka na mwanaume mwingine anayeitwa Jean de Dieu ambaye tulikuwa tukiimba pamoja katika kwaya. Walienda Gisenyi pamoja. Walitumia wiki mbili kwenye ufukwe. Walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na kufanya uzinzi," alisema Uwihoreye Francois

Wanandoa hao Warwanda walifanya harusi ya kortini ambayo haikuchukua muda au rasilimali nyingi kwani walirudi nyumbani haraka. Uwihoreye aliondoka nyumbani kwenda kazini baada ya harusi yao, akitumaini kupata kazi na kuweka pesa za harusi kubwa na ya kifahari. Hakuweza kusadiki yale ambayo mkewe alifanya muda mfupi baada ya ndoa yao, lakini wale waliomwona mkewe na mwanaume mwingine walimtumia picha.


Mwanamume huyo karibia apagawe kwa sababu hakuamini ujanja aliofanyiwa. "Baada ya wiki mbili hadi tatu, walirudi. Alikuwa amependana na mwanaume mwingine ambaye alikuwa yuleyule aliyekuwa na uhusiano naye. Yule mwanaume alimwambia afungue kesi ya talaka ili wao waweze kuolewa. Kwa hiyo, akanitaka talaka," alisema kijana huyo mwenye huzuni.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii