Ahukumiwa miaka miwili jela sababu ya Ex wake

Mchezaji soka wa Colombia na Klabu ya Boca Juniors, Sebastian Villa amehukumiwa miaka miwili na mwezi mmoja jela kwa kosa la kumnyanyasa kijinsia aliyekuwa mpenzi wake Daniela Cortes.

Daniela Cortes mpenzi wa zamani wa mchezaji huyo alimripoti mwezi Aprili mwaka 2020.

Hata hivyo milango ipo wazi kwa nyota huyo wa Boca Juniors kukata rufaa.

 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii