Mwanaume amtoa jicho shemeji yake kisa miti

Mwanamume aliyenaswa kwa kumjeruhi shemeji yake amepatikana na hatia kwa tuhuma zinazotolewa dhidi yake.

Janet Langa, mjane anayetoka Nyaori huko Nyalenda, kaunti ya Kisumu, alivamiwa kinyama na kakake marehemu mumewe mnamo Machi 13, kufuatia kuzuka kwa ugomvi kati yao.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 40 alikuwa amemzomea Isaac Onditi kuhusu kukata miti katika boma hilo na kujifaidisha na mapato yake bila kumgawa. Onditi alimshambulia Langa kwa kumrushia koleo usoni.

"Janet Langa alishambuliwa na nduguye mkwe katika eneo la Nyaori, Nyalenda baada ya kumhoji kwa nini alikata miti ya nyumbani na kuiuza, lakini hakumpa hata senti moja. "Tukio hilo liliripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Kasagam baada ya mama huyo wa watoto watatu kulazwa katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga ,



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii