olisi huko Mlolongo wanamzuilia mwanamke anayedaiwa kuhusishwa na genge la wizi wa watoto linaloendesha shughuli zake katika eneo hilo.
Miriam Wesonga mwenye umri wa miaka 18 alikamatwa na wananchi baada ya kuonekana akiwa na mtoto anayesadikiwa kuibiwa
Wesonga alipelekwa katika afisi ya chifu Mlolongo, ambapo alikiri kuwa mmoja wa genge la kuiba watoto na kuwauza Uganda kupitia Busia. Katika video ya runinga ya Citizen, chifu wa Mlolongo Peter Ndunda, alisema mshukiwa alikiri kuwa miongoni mwa genge la wanawake watatu wanaoiba watoto kutoka eneo la Mlolongo.
Ndunda, ambaye alimkabidhi mwanamke huyo kwa maafisa katika Kituo cha Polisi cha Mlolongo, alisema mwanamke huyo alifichua kuwa anapokea TZS 854,330.71kutoka kwa mshirika wake kwa kila mtoto aliyeporwa. "Alisema anapata TZS 854,330.71 kwa kila operesheni inayofanikiwa na ndiyo sababu nilimpeleka Kituo cha Polisi cha Mlolongo. Kulingana na uungamo wake, hadi sasa amepora watoto watatu, wawili kati yao wamepatikana huku mwingine angali anatafutwa. Hatujui ikiwa mtoto ambaye alipatikana naye ni wake kama anavyodai. Hii ni biashara, alisema, na anapata malipo kwa hilo. Bado hatujagundua ni nani washirika wake na kwa nini wanampeleka Uganda," Ndunda alisema.
Chifu wa eneo hilo alisema watekaji nyara wamekuwa wakiwapumbaza watoto kwa kuwapa peremende na vitafunio kabla ya kutoweka nao.