Watu watano wa familia moja wamekutwa wakiwa wameuawa nyumbani kwao eneo la Zanka wilayani Bahi mkoani Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Mkuu
wa Mkoa Dodoma Antony Mtaka pamoja na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani
Dodoma, Onesmo Lyanga wamefika eneo la tukio usiku wa kuamkia leo
ambapo miili ya watu hao imekutwa ikiwa ndani ya nyumba yao walimokuwa
wanaishi ikiwa tayari imeharibika.
Waliouawa katika tukio hilo ni Baba, mama, watoto wawili na mjukuu mmoja.
Akizungumza
mara baada ya kufika eneo la tukio, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony
Mtaka amelitaka Jeshi la Polisi mkoani humo kuanza uchunguzi mara moja
ili kubaini watu waliohusika kufanya mauaji ya watu hao watano wa
familia moja.
Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi kuhusu vifo hivyo, ikiwemo kubaini watekelezaji wa tukio hilo la kikatili