Kulingana na majirani, mwanamke huyo amekuwa akiwaleta wanaume hao kwake kwa zamu ila siku hiyo, ratiba yake ilifeli na wawili hao wakakutana usiku ule.
“Huwa anawaleta siku moja moja usiku sana na wanatoka asubuhi, sasa hawa wawili pia ni watu wanajuana, wako na urafiki na ni wakulima wageni mjini,” alieleza Esther Musangi ambaye ni jirani.
Duru za mtaani zinasema kwamba Hellen aliabiri gari na kutoka mji huo asubuhi akiwa amejitanda ili asitambulike.
Marafiki wa mwanamke huyo wanadai kuwa alirudi kwao, japo kwa mujibu wa mume wake, simu yake imesalia kuzimwa.
Bw Meso amekwisha beba bidhaa za nyumba na kuzisafirisha hadi mjini Malindi kwa ndugu yake.