Mtoto mwenye umri wa miaka 12, kutoka nchini Zambia amefariki dunia baada ya kudaiwa kupigwa na marafiki zake watatu wakati wakicheza mchezo wa mateke na makofi.
Kulingana na shangazi wa marehemu, Mary Kabaso, Francis Ngosa aliagizwa kuchota maji saa kumi jioni Alhamisi ya Mei 18, 2023, lakini alirejea nyumbani saa mbili usiku, huku akishindwa kutembea. Alipoulizwa kwa nini alishindwa kutembea na kuchukua muda mrefu kufanya kazi ambayo kwa kawaida ilikuwa ndogo, alijibu kwamba alikuwa akicheza na marafiki zake watatu ambao wanadaiwa kumpiga.
Inadaiwa usiku huo huo hali ya Ngosa ilidhorora na familia yake iliamua kumkimbiza katika Zahanati ya Luamfumu ambako alithibitishwa kuaga dunia.