Idadi ya waliofariki kwa kukaa njaa yafikia 226

Nchini Kenya, miili mingine 15 imepatikana katika msitu wa Shakahola, Pwani ya nchi hiyo na kufikisha idadi ya watu waliopatikana kufikia 226 wanaohusishwa na mchungaji mwenye utata Paul Mackzie aliyewahimiza wafunge hadi wapoteze maisha ili wamwone Yesu.

 Serikali imetangaza marufuku ya watu kutembelea wakati huu inapoendelea na msako zaidi, na hii hapa ni taarifa yake.

Wanavijiji hapa wanasema maisha yao imebadilisha baada ya amri hiyo kuwekwa. Taabu Kajole ni mzee wa nyumba kumi (kiongozi wa eneo) katika kijiji cha Binzaro Bofa, Shakahola pwani ya Kenya


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii