Mkewe Yesu wa Tongaren Sasa Awaomba Wakenya Kuisaidia Familia Yake

Nabii Benjamin, ambaye ni mke wake mhubiri Eliud Wekesa maarufu kama Yesu Wa Tongaren kutoka Bungoma, ameomba msaada kutoka kwa Wakenya. 

Katika kipande cha video kilichorekodiwa nyumbani kwake, mama huyo wa watoto wanane alisema maisha yamekuwa magumu tangu mumewe akamatwe. 

Aliwaomba wasamaria wema kumsaidia, akilia kwamba hawezi kumudu mahitaji ya chakula nyumbani. "Baada ya mume wangu, Yesu Wa Tongaren, kuwekwa ndani, maisha yamekuwa magumu. Yeye ndiye kimega mkate wetu. Kwa sasa, nimekwama na watoto kwa sababu sina chanzo cha mapato. Watoto wangu wanakufa njaa kwa sababu mimi ni maskini." 




Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii