Jamaa Amnunulia Mbwa Wake Gari Kusherehekea Siku Yake ya Kuzaliwa

Mwanaume mmoja raia wa Nigeria amemwandalia mbwa wake sherehe kubwa ya kufana kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na kumnunulia gari lenye thamani ya mamilioni ya pesa. 


Mwanamume huyo aliyetambuliwa kwa jina Doktor Skidon, alikuwa amewalika marafiki zake nyumbani kwake kumsherehekea mnyama huyo. 


Kilele cha sherehe hiyo kilikuwa wakati alipomzawadi mbwa huyo gari jipya. Alichagua kununua gari hilo kwa jina la mbwa huyo na kulitaja kama mtoto wake. 



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii