Nchini Kenya, idadi ya miili ya watu iliyofukuliwa katika eneo la Shakahola Pwani ya nchi hiyo, inayohusishwa na Mchungaji mwenye utata Paul Mackenzie, anayedaiwa kuwapotosha waumini wake kufunga chakula mpaka kufa ili kumwona Yesu, imeongezeka na kufikia 150.
Rhoda Onyancha, mwakilishi wa serikali katika eneo la Pwani anasema huenda miili zaidi ikapatikana baada ya watu wengi kuripoti kutowaona wapendwa wao.
“ Maofisa wetu wamefukuwa miili mitano zaidi lakini pia tumepokea taarifa ya watu ambao wanaowatafuta wapendwa wao na pia tumepokea taarifa kuwa watu 594 ambayo hawajapatikana na wanatafutwa na jama zao.” alisema Rhoda Onyancha, mwakilishi wa serikali katika eneo la Pwani.