Waziri
Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anayepigania kuinusuru kazi yake baada
kufanya sherehe za kunywa pombe ofisini na makazi yake ya Downing Street
kipindi nchi ilipokuwa imefungwa kutokana janga la virusi vya Corona,
ameliambia bunge leo kwamba hatojiuzulu
Johnson ana wakati mgumu kutuliza hali hata ndani ya chama chake ambapo baadhi ya wabunge walioghadhabi shwa na sherehe hizo wanamtaka aachie ngazi.
Huku hayo yakiarifiwa, Waziri Mkuu huyo amesema kuwa watu nchini England hawatohitajika kuvaa barakoa mahali popote au kufanyia kazi nyumbani kuanzia wiki ijayo.
Johnson amesema wanasayansi wanaamini kwamba wimbi la kirusi cha Omicron limesambaa kote nchini humo. Ameongeza kwamba hatua ya kuonyesha vyeti vya chanjo ya corona itafikia kikomo pia ingawa biashara zitaamua iwapo zitaendelea na utaratibu huo au la.