Mahakama Yamwachilia Mwanamume Baada ya Kumfunga Miaka 33 Kimakosa

Mwanamume mmoja nchini Marekani ameachiliwa na Mahakama ya California baada ya kutumiwa kifungo cha miaka 33 kwa tuhuma za jaribio la mauaji.

Fox 2 inaripoti kuwa Daniel Saldana mwenye umri wa miaka 55 alikuwa mmoja wa watu watatu walioshtakiwa kwa tukio la kupigwa risasi karibu na shule ya upili mwaka 1990. 

Mwendesha mashtaka wa Los Angeles George Gascón anasema jimbo lilifungua upya kesi yake na kubaini kuwa hakuwa mhusika katika mauaji hayo. "Najua kuwa hii haitarudisha miongo uliyoishi gerezani. Lakini natumai kuwa ombi letu la msamaha linakuletea faraja kidogo wakati unaanza maisha mapya," Gascón alisema.

Baada ya miaka sita tangu ushahidi ulipotolewa, Saldana alitangazwa kuwa hana hatia, alisema Gascón. Kucheleweshwa kulitokana na naibu mwendesha mashtaka wa zamani ambaye alikuwepo kwenye kikao cha kuachiwa ambapo mshitakiwa alitoa ushahidi wa kuondolewa mashtaka. Inaonekana kuwa afisa huyo hakutumia ushahidi au kumjulisha Saldana na wakili wake, kama inavyotakiwa na sheria. Saldana alionekana na Gascón katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi, akisema kuwa anashukuru kuwa huru. 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii