Mwanafunzi Achoma Bweni na Kuua Wanafunzi 19 Kisa Kunyang'anywa Simu

Msichana mwenye umri wa miaka 15 ameshtakiwa kwa kuchoma moto bweni la shule huko Guyana na kusababisha vifo vya wanafunzi 18 na mvulana wa miaka mitano.
.
Msichana huyo alishtakiwa siku ya Jumatatu kwa makosa 19 ya mauaji, Atashtakiwa kama mtu mzima mahakama karibu na mji mkuu wa Georgetown iliamua kulingana na #AssociatedPress.
.
Polisi wanadai msichana huyo alichoma moto kwa makusudi Mei 21 kwa Shule ya Sekondari ya Mahdia kulipiza kisasi baada ya afisa wa shule hiyo kumpokonya simu yake ya Mkononi.
.
Polisi wanasema milango yote mitano katika jengo lililoungua ilikuwa imefungwa kwa funguo ndani Huku Msimamizi wa bweni anasemekana kufunga milango yote ni kama tahadhari kuzuia wanafunzi wa kike wenye umri wa kuanzia miaka 12-18 kutoka kwa siri kwenda kujumuika na wanaume watu wazima katika mji wa karibu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii