MWANAMUZIKI MEGAN STALLION AONEKANA AKIJIVINJARI NA MWANSOKA LUKAKU


Inafahamika kuwa megan Stallion amekuwa katika vichwa vingi vya Habari kufuatia lile Sakata dhidi yake na mwimbaji tory lanez.

Fununu zilizosambaa katika mitandao mbali mbali ya kijamii ni kufuatia megah stallion kuonekana akijivinjari na nyota wa soka wa Ubelgiji Romelu Lukaku kwenye harusi ya mmoja wa wachezaji wenzake.

 

Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, wawili hao walionekana wakiwa wamekaa karibu na kila mmoja walipokuwa wakisherehekea harusi ya Lautaro Martínez – wa klabu ya Inter Milan ya Italia - na mkewe wakifunga pingu za maisha kwenye sherehe ya kifahari huko Cernobbio, Italia siku ya Jumatatu. 

Klipu nyingine ilimnasa Megan na Romelu wakipiga soga kwa faragha huku wakiangalia mandhari ya kuvutia ya Ziwa Como, na hivyo kuchochea tetesi za kuwa kuna mahaba kati yao.


Ingawa haijulikani ikiwa Megan alihudhuria harusi hiyo kama Rafiki wa Lukaku, au inafaa kusema kwamba wote wawili walikwenda kwa sababu ya ukaribu wao na lebo ya  Roc Nation ya JAY-Z.

Megan alisaini mkataba wa usimamizi na kampuni ya Powerhouse mwaka 2019, huku mfungaji mabao huyo wa Ubelgiji akiwa mchezaji wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza kujiunga na Roc Nation Sports mnamo 2018, wakati huo alikuwa akiichezea Manchester United.

Uhusiano wao wa kikazi unaongezeka zaidi kwani Houston Hottie ni balozi mashuhuri wa Nike, ambaye Lukaku anavaa nguo zake kwa sasa uwanjani baada ya ushirikiano wake uliovunja rekodi wa Puma kukamilika kimya kimya miaka mitatu iliyopita.

 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii