CAMILA CABELLO NA SHAWN MENDES WAAMUA KUJARIBU NAFASI NYINGINE

Wapenzi wawili ambao waliwahi kutikisa katika safu ya burudani wakiwa Pamoja shawn mendes Pamoja na mwanadada camia Cabello wameamua kurudi Pamoja na kuangali pale walipokosea mpaka kuamua kuvunja mahusiano yao  ambayo walianza kuwa Pamoja mwaka 2019.

Camila na shawn mendes  mapema mwaka huu wamefanikiwa kukutana katika tamasha ya muziki la Coachella na wawili hao wameonekana wakikumbatiana Pamoja na kupena mabusu jambo ambalo limedhihirisha kuwa wawili hao wameamua kuweka tofauti zao pembeni.


Mapema jumanne hii wawili hao wameonekana Pamoja huko jijini new York wakiwa katika mtoko wa Pamoja huku wakiwa wenye furaha na wameshikana mikono.

Ikumbukwe kwamba wawili hao walivunja mahusiano yao novemba mwaka 2021 na ikasemekana shawn aliamua kuingia katika mahusiano na daktari wake ambaye anafahamika kwa jina la dr.jocelyne miranda.

Lakini bado hawajaweka wazi rasmi kama wameamua kurudia au ni urafiki tu.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii