Fundi Ujenzi, Iddi Saidi Kindula (37), mkazi wa Madale jijini Dar es Salaam anadaiwa kumuua mkewe, Tukae Seif Ramadhani (16), kwa kumnyonga kisha naye kukutwa amefariki dunia akining’inia kwenye kamba chumbani kwao huku wakikiacha kichanga cha miezi minne kikiangua kilio muda mrefu bila msaada.
Tukae ambaye kwa sasa angekuwa kidato cha kwanza, ndugu zake wamesema alikataa shule kwa ajili ya kuolewa na mwanaume huyo asijue kama mapenzi hayo yangeweza kumbadilikia ndani ya kipindi kifupi akiwa na umri huo mdogo.
msiba wa mwanaume huyo umehamishiwa kwa ndugu zake na msiba wa Tukae umehamishiwa kwa wazazi wake ambapo mwanahabari wetu alielekezwa na kufika.
Ndugu walijawa na huzuni wakiwa na kichanga kilichoachwa yatima na kifo cha kinyama kilichowakuta wazazi wake.