Mwanamke Afariki Dunia Ndani ya Basi Akielekea Kilifi Kusaka Maombi

Mwanamke mmoja aliyefunga safari kutoka Bungoma kuelekea Mombasa kutafuta maombi, alifariki dunia akiwa ndani ya basi. 


Kwa mujibu wa ripoti ya polisi ya kituo cha Polisi cha Central, dereva wa basi la Simba Coach, Musa Moi Owalo alipiga ripoti kuwa Consolota Wesonga Otieno alikuwa akisafiri kutoka Bungoma kuelekea Mombasa alipofariki njiani. 


Polisi walitembelea eneo la tukio na kupata maiti ya mwanamke huyo. Baada ya kupekua mkoba wake, polisi walipata hati kadhaa za matibabu zilizoonyesha kuwa mwanamke huyo alikuwa akiugua maradhi yasiyojulikana. 



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii