Jela miaka 30 kwa kumbaka mwanae

Mchungaji Nurdin Abdallah ambae ni muinjilisti wa vitabu amehukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka kwa nyakati tofauti binti yake mwenye umri wa miaka 6.

Akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi mwandamizi Erick Kimaro wa mahakama ya wilaya ya Magu amesema mahakama hiyo imejiridhisha pasipo kuwa na shaka kwamba mshtakiwa huyo ametenda kosa hilo

Ushahidi huo umethibitishwa  kupitia mashahidi ambao ni mtoto aliyekuwa anabakwa pamoja na Ushahidi wa daktari aliyeithibitishia mahakama hiyo kuwa ni kweli sehemu za siri za binti huyo zilikuwa zinaonesha ameingiliwa


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii