Binti Afariki Katika Mazishi ya Babake

Msiba ulitokea kwenye hafla ya mazishi katika eneo la Mukumu, kaunti ya Kakamega, baada ya mwanafunzi mwenye umri wa miaka 11 kwa jina Benta kufariki kwenye mazishi ya baba yake. 

Jamaa wa familia hiyo wanasema kwamba msichana huyo aliyekuwa na huzuni alilalamikia maumivu ya kichwa na kuzirai muda mfupi baadaye hali iliendelea kuwa mbaya.


Juhudi za kuokoa maisha yake kwa kumkimbiza katika kituo cha afya kilicho karibu hazikufua dafu kwani alitangazwa kuwa amefariki alipofika

Mjane huyo alifichua kuwa mwendo wa saa 9 asubuhi wakati kila mtu alikuwa akijiandaa kwa maziko, binti yake alianza kulalamikia kuumwa na kichwa. 

Msichana huyo alipoanguka na kuzimia, familia ililazimika kusimamisha ibada ya mazishi ili kumkimbiza hospitalini. "Sijui hata nianzie wapi kwani nimeachwa na watoto tisa wa kuwalea pekee yangu," mjane huyo aliyejaa huzuni alisema Ripoti zinaonyesha kuwa mwanamume huyo alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi, na bintiye alifuata vivyo hivyo siku ya mazish yake. Jamaa wa familia hiyo waliwaomba wasamaria mema kujitokeza kumsaidia mjane huyo kusomesha watoto walioachwa.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii