Maporomoko ya ardhi kaskazini mwa Pakistan yafukia malori 20

Malori yapatayo 20 yamefukiwa kwenye mporomoko ya ardhi kaskazini magharibi mwa Pakistan. Hali hiyo ilitokea baada ya barabara kuu inayopitia katika eneo la Khyber kukumbwa na mvua kubwa zilizosababisha dhoruba kali.

Malori yapatayo 20 yamefukiwa kwenye mporomoko ya ardhi kaskazini magharibi mwa Pakistan. Hali hiyo ilitokea baada ya barabara kuu inayopitia katika eneo la Khyber kukumbwa na mvua kubwa na radi  zilizosababisha dhoruba kali. 

Naibu kamishna wa wilaya hiyo ya Khyber Abdul Nasir Khan ameliambia shirika la Habari la Reuters kwamba raia wawili wa Afghanistan wamekufa na watu wengine watatu wamepelekwa hospitalini huku wakitarajia idadi ya watu waliojeruhiwa kuongezeka. Amesema kazi ya uokoaji inaendelea.

Maporomoko hayo ya ardhi yalitokea alfajiri ya leo Jumanne katika njia kuu inayounganisha Pakistan na Afghanistan.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii