Takribani watu 200 wauwawa nchini Sudan

Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa wito kwa pande zinazopigana nchini Sudan kusitisha mara moja uhasama huku mjumbe wake mjini Khartoum akisema takriban watu 200 wameuawa na mapigano hayo

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alisema kuongezeka kwa mzozo kati ya jeshi na vikosi vya kijeshi, wakiongozwa na majenerali wapinzani kunaweza kusababisha hali mbaya kwa nchi na eneo hilo kwa ujumla.

Vurugu hizo, zilizozuka Jumamosi, ziliendelea, huku idadi ya vifo ikiongezeka na watu wasiopungua 185 wakitajwa kupoteza maisha, Volker Perthes, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, aliwaambia waandishi wa habari.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii