AJINYONGA JUU YA GOLI

Tyson Kilasi (32), Mkazi wa Kijiji cha Mawindi Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe, amekutwa amefariki kwa kujinyonga kwenye goli la kuchezea mpira wa miguu wa kijiji hicho huku pembeni akiwa ameacha nguo ya ndani ya kike.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mawindi Kata ya Igima, Elias Mwinami amethitibitisha kutokea kwa kifo cha Kijana huyo na kusema kifo hicho kimetokea usiku wa kuamkia January 18,2022.

Mwinami amesema chanzo cha kifo cha Kijana huyo bado hakijafahamika ambapo eneo ambalo mwili wa Kijana huyo wameukuta ni eneo la goli la mpira wa miguu na wamekuta nguo ya ndani ya Mwanamke.

“Tumemkuta ananing’inia kwenye goli lakini chanzo bado hakijafahamika na kimsingi tunalaani kitendo hiki ifike mahali tuelimike na hivi karibuni tu Poliai walikuja kutoa elimu kwa kweli wananchi waache kujichukulia sheria mkononi"

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii