Idadi ya vifo nchini DRC imefikia zadi ya watu mia tano kutokana na mafuriko na kufunikwa na maporomoko ya matope yaliyosababishwa na mvua kubwa za siku nne mfululizo, huko Nyamukubi Wilayani Kalehe jimbo la Kivu kusini.
Mvua hizo, pia zimesababisha uharibifu wa nyumba, na kufanya maafa makubwa kuwahi kutokea katika historia ya hivi karibuni huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.