Wanawake Waliozaa na wakandarasi Wa China Haya Ndio Yanayowakuta Wanawake Hao

Kwa zaidi ya muongo uliopita, Wachina wamekuwa wakifurika mijini na vijijini barani Afrika kujenga barabara, mabwawa, madaraja na miundombinu mingine ya kisasa.

Hata hivyo, kuja kwao kumeleta baraka na masaibu kutokana na kuhusika katika mauhusiano ya kimapenzi na wenyeji na matokeo kuwa watoto wa rangi tofauti.


Lakini tatizo ni kwamba wanawake waliozaa watoto na Wachina hao hujipata kwenye njia panda baada ya mradi huo wa ujenzi kumalizika na raia hao wa kigeni kuondoka. 

Watoto waliozaliwa kutokana na mahusiano hayo pia wana ugumu wa kutangamana na wenzao kwa sababu wanaonekana tofauti sana na wakati mwingine husababisha wao kudhihakiwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii