Mfadhili wa Mbegu za Kiume Aliyezaa Watoto 550 Kote Duniani, Ashtakiwa kwa Kuzaa Sana

Mwanamuziki wa Uholanzi mwenye makazi yake nchini Kenya na ambaye ni mfadhili mkubwa wa mbegu za kiume aliyezaa takriban watoto 550 duniani kote anakabiliwa na mashtaka.

Jonathan Jacob Meijer, 41, ameshtakiwa kwa madai ya kuongeza hatari ya uhusiano wa kingono kati ya ndugu wa damu.

Kwa mujibu wa gazeti la New York Post, Meijer, amefadhili mbegu za kiume katika angalau kliniki 13, zikiwemo 11 za Uholanzi, ambapo aliwekewa vikwazo mwaka wa 2017 kwa kuzaa watoto 102.


Kulingana na sheria za Uholanzi, wafadhili wa manii hawaruhusiwi kuzaa zaidi ya watoto 25 au kuwapa mimba zaidi ya wanawake 12 ili kuzuia kuzaliana, uhusiano wa ujamaa au matatizo ya kisaikolojia kwa watoto wanaogundua kuwa wana ndugu na dada wengi.

Lakini licha ya vikwazo hivyo, Meijer anandelea kutoa mbegu zake nje ya Uholanzi, ikiwa ni pamoja na Denmark na Ukraine. Haya ni kulingana na Wakfu wa Uholanzi wa DonorKind, ambao umemshataki mwanamziki huyo. Kundi hilo linadai kuwa mfadhili huyo wa mbegu za kiume amekuwa akidanganya kuhusu idadi ya watoto aliowazaa. Kesi hiyo iliwasilishwa na mwanamke Mholanzi ambaye ni mmoja wa waliomzalia Meijer watoto mwaka wa 2018

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii