Aiba mtoto na akamdanganye mume wake

Mahakama ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza imemhukumu kifungo cha miaka miwili gerezani Happyness William mwenye umri wa miaka 18 mkazi wa Nyehunge wilayani humo kwa kosa la wizi wa mtoto wa miezi sita.


Ni kesi ya wizi wa mtoto namba 64 ya mwaka huu ambayo imetajwa kwa mara ya kwanza katika mahakama ya wilaya ya Sengerema mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Tumsifu Barnabas ambapo mshtakiwa Happiness William mara baada ya kusomewa shtaka linalomkabili la wizi wa mtoto alikiri kutenda kosa hilo ndipo mahakama ikatoa hukumu hiyo

Awali mwendesha mashataka wa serikali Mkaguzi wa polisi Inspector Martha Chacha aliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe 26 ya mwezi huu majira ya saa mbili asubuh katika mtaa wa Migombani kata ya Nyampulukano tarafa ya Sengerema wilayani Sengerema mwanamke huyo alimuiba mtoto aitwaye Anitha Richard mwenye umri wa miezi sitana Kwenda nae katika Kijiji cha Nyehunge ili akamuonyeshe mume wake kuwa amejifungua na kwamba huyo ndiyo mtoto wake

Aidha mwendesha mashtaka huyo wa serikali ameongeza kuwa mwanamke huyo kabla ya kumuonyesha mume wake mtoto huyo alikamatwa na jeshi la polisi na kufunguliwa shtaka la wizi wa mtoto, ambalo ni kinyume na kifungu namba 169 kifungu kidogo cha (1) (a) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 ndipo mahakama ya wilaya ya Sengerema ikamhukumu kifungo hicho cha miaka miwli gerezani

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii