Kiongozi wa Muungano wa Azimio La Umoja One Kenya Raila Odinga amesisitiza kuwa safari yake ya kwenda Ikulu haiwezi kuzimwa.
Kupitia kitandazi chake cha Twitter baada ya maandamano hayo, Raila alimkemea Naibu Rais Rigathi Gachagua akimshutumu kwa kuamuru polisi kuwadhuru wafuasi wake. "Chini ya maagizo ya Rigathi, ukatili wa polisi dhidi ya waandamanaji wa amani umeongezeka leo. Azimio letu, kwa upande mwingine, limeongezeka kutoka hatua moja hadi nyingine."
"Tunataka kuhakikishia utawala haramu kwamba tutaonana nao peupe mapema Alhamisi kote nchini," Raila alichapisha kwenye Twitter. Haya yanajiri huku baadhi ya viongozi wa kidini kutoka Nyeri wakimtaka Raila kusitisha maandamano hayo ya kuipinga serikali kote nchini. Kulingana na wahubiri hao, maandamano hayo sio mazuri kwa Wakenya kwani yanapoteza muda, rasilimali na hata maisha ya watu wasio na hatia.
Maandamano Yataendelea Alhamisi Mapema Asubuhi.