Russia inasema imezuia shambulio la ndege isiyo na rubani ya Ukraine

Mifumo ya ulinzi wa anga ya Russia Jumapili imezuia shambulio la ndege isiyo na rubani ya Ukraine katika mji mmoja wa Russia ambapo watu watatu walijeruhiwa na majengo ya makazi kuharibiwa, wizara ya ulinzi ya Russia imesema.

Kyiv haikujibu mara moja ombi la Reuters la kutoa maelezo juu ya shambulio hilo. Awali ilikanusha madai ya Russia kwamba ndege zake zisizo na rubani ziliingia kwenye anga ya Russia na kusababisha uharibifu kwenye miundombinu ya kiraia.

Taarifa ya wizara ya ulinzi imesema shambulio katika mji wa Kirevevsk umbali wa kilomita 220 kusini mwa Moscow, lilihusisha drone ya Ukraine aina ya Tu-141.

Shirika la habari la Russia, Tass, limenukuu maafisa wa eneo hilo wakisema kuwa watu watatu walijeruhiwa katika tukio hilo. Tass imesema nyumba tano za watu binafsi ziliharibiwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii