Wanamgambo mashariki mwa DRC wauwa watu wapatao 15

Afisa kutoka shirika moja la kiraia kwa jina Charite Banza amefahamisha kwamba wapiganaji wa kundi la waasi la CODECO walishambulia kijiji cha Drodro katika mkoa wa Ituri kwenye mji wa Djungu siku ya Jumatano.

Watu sita waliuwawa kwa kukatwakatwa kwa mapanga, na wengine watatu waliuawa katika kijiji kingine kilichoko umbali wa kiasi kilomita 30.

Kwa upande mwingine, wanamgambo wa kundi la Allied Democratic Forces-ADF nao walishambulia jana Alhamisi katika mkoa wa Ituri na kuuwa raia sita, kwa mujibu wa mfanyakazi mmoja wa shughuli za kutoa msaada aliyeomba kutotajwa jina.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii