Aliyekuwa mwanasiasa wa India ameuawa kwa kupigwa risasi akizungumza moja kwa moja kwenye runinga pamoja na kaka yake.
Atiq Ahmed, ambaye alikuwa chini ya usalama wa maafisa wa polisi, alikuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati bunduki ilipotolewa karibu na kichwa chake mjini Prayagraj. Katika video ilisombaa, Ahmed na kaka yake, Ashraf, wote walikuwa wamefungwa pingu, wakizungumza na waandishi wa habari wakiwa njiani kwenda kuchunguzwa afya zao hospitalini sekunde chache kabla ya wote wawili kupigwa risasi.
Ahmed, ambaye alipatikana na hatia ya utekaji nyara, alifyatuliwa risasi Jumamosi, Aprili 15 usiku, na wanaume watatu waliokuwa wakijifanya wanahabari,
Wanaume hao walijisalimisha haraka na kuwekwa chini ya ulinzi. Ahmed, kando na utekaji nyara alikuwa akikumbana na kesi ya mauaji na unyang'anyi, katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.
Mahakama ya India ilimhukumu yeye na wengine wawili kifungo cha maisha mnamo Machi mwaka huu katika kesi ya utekaji nyara. Mauaji yake yanajiri siku chache baada ya mwanawe kuawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Kifo chake pia ni baada ya Ahmed kudai hapo awali kwamba alikuwa akitishiwa maisha na polisi.