Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimeitaka serikali kuunda tume ya kijaji kushughulikia sakata la Plea Bargaining ambalo limetajwa kwenye ripoti ya CAG kuwa zoezi hilo liliendeshwa kwa kukiuka sheria.
Akizungumza na wanahabari John Mnyika ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho amesema kwa inavyoonekana kwa sasa jambo hilo limeachwa kwa tume ya haki jinai iliyoundwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan jambo ambalo anasema sio sahihi
"Tunatoa wito kwa Serikali kuunda Tume ya kijaji kushughulikia jambo hili la Plea Bargaining." amesema