Mahakama nchini Nigeria imempa mwanamume mmoja makataa ya hadi Ijumaa, Aprili 7, kumuua jogoo wake kufuatia malalamishi ya jirani yake kuwa kuwika kwa ndege huyo kulikuwa kukimharibia usingizi.
Hakimu wa Mahakama ya Kano alimwamuru Malam Yusuf siku ya Jumanne, Aprili 4, kumchinja jogoo huyo kwani kero kwa jirani yake.
Yusuf alijitetea akiambia mahakama hiyo kuwa alimnunua jogoo huyo kusherehekea Ijumaa Kuu na hivyo kuomba kupewa hadi siku hiyo takatifu ndipo aweze kumchinja na kufurahia pamoja na familia yake. Hakimu alikubali ombi lake ila kwa masharti kwamba kumzuia jogoo huyo kuranda randa katika makazi ya watu na kuwasumbua.