Akata nyeti zake baada ya kutengwa na familia

Anselum Sebuka mwenye umri wa miaka 42 mkazi wa Kijiji na kata ya Namagondo wilayani Ukerewe mkoani Mwanza amekutwa ndani ya chumba chake akiwa amejaribu kukata sehemu zake za siri kwa kutumia kisu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema mwanaume huyo alikuwa anatuhumiwa na ndugu zake kuiba mali mbalimbali za familia yake na za jamii inayomzunguka na kwenda kuziuza pamoja na ulevi uliokithili ambapo waliamua kumtenga kutokana na tabia zake

Baada ya tuhuma hizo ndipo aliamua kujikata uume wake kwa kisu na kuacha unaning’inia kwa lengo la kujiua
Kamanda Mutafungwa amesema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kifamilia uliopelekea mhanga kupata msongo wa mawazo na kwamba mwanaume huyo alipelekwa katika Hospitali ya wilaya ya Ukerewe kwa ajili ya kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kufuata njia sahihi za kutatua matatizo yao hususani kuwaona wataalamu wa afya ya akili ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na msongo wa mawazo na kukosa uvumilivu wa migogoro mbalimbali katika jamii

Katika tukio lingine kamanda Mutafungwa amesema Mathayo Mishaka, miaka 40, Mkulima na mkazi wa kijiji cha Sumaha kata yaw ala wilayani Kwimba anashikiliwa kwa tuhuma za kumpiga na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia kifo binti yake aitwaye Milembe Mihayo mwenye umri wa miaka 11

Aidha kamanda Mutafungwa ametoa wito kwa wazazi na walezi kuacha kutoa adhabu za kikatili kwa watoto wao na badala yake watumie njia sahii ya kuwaonya pindi wanapokose ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii